Super Woman - Nathassia Club Mix Instrumental

de Diamond Platnumz

Ayolizer
Aliumba ardhi akaumba mbingu
Akaumba mbalamwezi
Akaumba nafsi, akaumba wivu
Akayaumba na mapenzi
Na kukuacha sidhani, siwezi jaribu
Maana penzi kwa mzani, limenizidi mahbibu
Shika vyema usukani, twende taratibu
Nakuita sweety, ah roterote

Baada ya tuta baby koleza gear

Yaani tamtam kama pipi
Nakuita sweety, ah roterote
Fundi kwenye kwichikwichi
Shepu vipi? Kama lote
Vicheche nishadelete
Sitaki cheat, watoketoke
Kwenye moyo nimekupa seat
We ndIo dereva, asa kukuacha ooh oooh!

Naanzaje? Ooh mimi
Naanzaje? Aah mimi apa
Naanzaje? Mwenzako ooh kukuacha siwezi
Naanzaje? Ooh mimi
Naanzaje? Aah mi jamani
Naanzaje? Kukuacha ooh, kabisa siwezi

Hadithi kuja hadithi njoo, utamu kolea
Mwezenu huba liko kwa roho, limeninogea
Vishanshuda poleni ooh, mnalo wambea
Mtaja kuugua makwasha koo, kwa kutuongelea
Tena mie kwake ndio dakitari, nampa tiba halali
Wanaitaga sukari, alamba aam!
Na jana nilifunga nikasali, nikamuomba Jalali
Atuepushe madhohari, ya wanadam

Ah ah, we mtamtam kama pipi
Nakuita sweety, ah roterote
Fundi kwenye kwichikwichi
Shepu vipi? Kama lote
Vicheche nishadelete
Sitaki cheat, watoketoke
Kwenye moyo nimekupa seat
We ndio dereva, asa kukuacha ooh oooh!

Naanzaje? Ooh mimi
Naanzaje? Aah mimi apa
Naanzaje? Mwenzako ooh kukuacha siwezi
Naanzaje? Ooh mimi
Naanzaje? Aah mi jamani
Naanzaje? Kukuacha ooh, kabisa siwezi

Na kukuacha sidhani
Siwezi jaribu
Maana penzi kwa mzani
Limenizidi mahbibu
Wasaafi!

Más canciones de Diamond Platnumz